Kuhusu mkataba, Ajibu amekaushia kwanza kwa sababu akili yake inafikiria kitu kimoja tu kwa sasa
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu, ameweka masuala yote ya
kimkataba pembeni ili kuhakikisha anaifanikisha timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi kuu bara kutokana na ushindani uliopo hivi sasa.
Simba inaongoza katika msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55 lakini kama Yanga wangeshinda jana mechi dhidi ya Mtibwa Sugar basi wangepanda kileleni, lakini hata hivyo mambo yalikua tofauti na kuifanya Simba kuendelea kuongoza usukani huku zikiwa zimebaki mechi sita kwa kila timu kabla ya ligi kumalizika.
Ikumbukwe, Ajibu aliingia katika mgogoro na uongozi wake hivi karibuni kufuatia kugomea kuingia mkataba mwingine hadi pale atakapomaliza mkataba wake, ikiwa ni pamoja na kuugomea uongozi wake huo pindi ulivyomfuata kwa mara ya pili ili kuingia mkataba mpya, Mkataba wa Ajibu unamalizika mwishoni mwa msimu.
Ajibu mwenyewe amefunguka kwamba anaweka pembeni masuala ya kimkataba na anafanya kazi moja tu ya kuhakikisha anaisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa.
"Sasa hivi mtazamo wote upo katika kutwaa ubingwa wa ligi, hivyo suala la mkataba wangu na Simba kwa sasa naliweka pembeni na ninachokiangalia ni kuhakikisha timu yangu inatwaa ubingwa msimu huu kwani tumekuwa tukiusaka kwa muda mrefu.
"Ila sijajua kama nitaongeza ama la, cha msingi ni kuangalia hiki kilichopo mbele yetu ili kuweza kujijengea heshima," alisema Ajibu.
Kuhusu mkataba, Ajibu amekaushia kwanza kwa sababu akili yake inafikiria kitu kimoja tu kwa sasa
Reviewed by Steve
on
Monday, March 06, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, March 06, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment