Ishu kamili ya Pluijm kuondoshwa Jangwani ipo namna hii
Rasmi klabu ya Yanga imemtimua mkurugenzi wake wa ufundi, Hans van Der Pluijm kwa kile kilichoelezwa kuwa kubana matumizi na kuendana na hali halisi ya kiuchumi kwa sasa.
Kigogo mmoja ndani ya Yanga alithibitisha taarifa hizo kwa kusema; "Ni kweli tumeamua kuachana na Pluijm kwa mambo mawili, kwanza hali ya kiuchumi.
"Pili ni kuweka amani ndani ya timu maana mambo yalikua mengi, hivyo tumeona bora tuachane na katibu mkuu (Mkwasa) ndiye tuliyempa jukumu la kumtaarifu Pluijm kuhusu hali hii.
"Kubaki na Pluijm ni gharama kubwa na kama unavyoona hali ya uchumi sasa si nzuri sana na tumeona busara kuachana naye ili mambo mengine yaende."
Miongoni mwa gharama ambazo Yanga imekuwa ikiingia kwa kuwa na Pluijm ni kumlipa mshahara wa dola 10,000 zaidi ya Sh milioni 22 kwa mwezi, pia gharama nyingine za nyumba na usafiri.
Pluijm mwenyewe alipotafutwa, alisema: "Naomba jambo hilo aulizwe katibu mkuu wa timu, mimi sina la kusema."
Ishu kamili ya Pluijm kuondoshwa Jangwani ipo namna hii
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 04, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment