Propellerads

Masau Bwire amtetea Chirwa wa Yanga



Afisa habari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ameibuka na
kutetea bao la mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akitamka ni bao halali na mwamuzi Ahmed Simba amemnyima.

Kauli hiyo aliitoa dakika chache tangu mechi ya Ligi kuu Bara na Yanga imalizike kwa Ruvu kufungwa kwa mabao 2-0 mchezo uliopigwa Jumatano wiki hii Uwanja wa taifa Dar es Salaam.

"Tuwe wakweli mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ile aliuvuruga mchezo mchezo mzima kutokana na maamuzi yake aliyokuwa anayatoa wakati mechi hiyo inaendelea uwanjani.

"Kati ya upungufu aliouonyesha ni ule wa kukataa bao la Chirwa ambalo lililokuwa halali kabisa, nimeshindwa kuelewa sababu ya kulikataa bao lile, Chirwa alikuwa ameushika au aliotea kiukweli nimekosa majibu, lile bao lilikuwa halali kabisa.

"Kwa upande wetu Ruvu, mwamuzi alituonea kwa kuwapa Yanga penalti kitu ambacho siyo sahihi," alisema Bwire.
Masau Bwire amtetea Chirwa wa Yanga Masau Bwire amtetea Chirwa wa Yanga Reviewed by Steve on Saturday, March 04, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.