Propellerads

Ili kuhakikisha ushindi mechi za Simba zilizosalia, Aveva athibitisha kuondolewa kwa 'wasaliti'



Klabu ya Simba imedai kwamba ina uhakika wa kushinda mechi zao zilizobakia zikiwamo zile za Kanda ya Ziwa na kunyakua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, baada ya kufanikiwa kuwaondoa wasaliti wote kwenye timu yao.

Akiweka wazi maandalizi  kuelekea mechi mbalimbali zilizobaki za Ligi Kuu Bara, Rais wa Simba, Evans Aveva alisema wana imani watashinda kwa sababu kikosi hicho hakina wasaliti na wanapambana kila eneo kuhakikisha wanaibuka na pointi tisa kwa michezo yao hasa ya kanda ya Ziwa.

"Kwa sasa hatuna wasaliti kwenye kikosi chetu, hivyo mechi za kanda ya Ziwa tutapambana kuhakikisha tunaibuka na ushindi ambapo nadhani haitakuwa shida sana kwa sababu hakuna usaliti," alisema.

Aveva alipotakiwa kueleza kwa kina ni wasaliti gani ambao wamewaondoa kwenye kikosi hicho, aligoma na kudai ni jambo la ndani.

"Hayo mambo ya 'virusi' ni mambo ya ndani, ila kikubwa kila mechi yetu kwa sasa ni fainali, hatuwezi kudharau kitu, hivyo mechi zilizosalia ni wajibu wetu kushinda ili kuhakikisha tunasonga mbele na kutimiza lengo letu la kunyakua ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA msimu huu," alisema.
Ili kuhakikisha ushindi mechi za Simba zilizosalia, Aveva athibitisha kuondolewa kwa 'wasaliti' Ili kuhakikisha ushindi mechi za Simba zilizosalia, Aveva athibitisha kuondolewa kwa 'wasaliti' Reviewed by Steve on Thursday, March 23, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.