Pamoja na dili la Sweden kukwama, Ndemla bado anafikiria Ulaya tu...mwenyewe amefunguka hapa
Kiungo wa Simba, Said Ndemla amesisitiza atakwenda kucheza soka Ulaya pamoja na dili lake la Sweden kukwama.
Ndemla amefunguka kwamba hajakata tamaa ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania, kwani atahakikisha ndoto yake inatimia.
Ndemla alisema bado anafikiria kucheza soka ya kulipwa na meneja wake anaendelea kumtafutia timu ya kuchezea.
Alisema atakuwa tayari kwenda kucheza soka katika nchi yeyote ili aweze kutimiza malengo yake aliyojiwekea.
"Si kama nimekata tamaa, lengo langu la kucheza soka nje liko pale pale na ninaamini kuna ofa tayari meneja wangu atakuwa amezipata sema sijakutana naye hivi karibuni kutokana na kubanwa na ratiba za mechi," alisema Ndemla.
Mwezi uliopita, Ndemla alishindwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC ya Sweden anayocheza Mtanzania, Thomas Ulimwengu, inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, kwa madai ya kukosa ruhusa kutoka kwa klabu yake ya Simba.
Pamoja na dili la Sweden kukwama, Ndemla bado anafikiria Ulaya tu...mwenyewe amefunguka hapa
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 23, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment