Propellerads

Achana na ya mtaani, haya hapa maneno kutoka uongozi wa Simba kuhusu Yanga kutolewa Ligi ya Mabingwa




Uongozi wa Simba umesema kuwa kitendo cha Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kimewaumiza sana.

Yanga ilitupwa nje katika michuano hiyo na Zanaco ya Zambia baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hapa nyumbani na kwenda Zambia ambako wikiendi iliyopita walitoka suluhu na hivyo kuondolewa kwa bao la ugenini.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', amefunguka kwamba uongozi wa Simba haukupenda Yanga itolewe katika michuano hiyo kwa sababu ilikuwa ikiiwakilisha nchi, hivyo kutolewa kwao ni pigo kubwa.

"Sisi kama Simba hatukufurahishwa kabisa na hali hiyo iliyowatokea Yanga, kwani tumeumia tukiwa kama Watanzania ambao tulikuwa tukiiombea ifike mbali katika michuano hiyo.

"Hata hivyo, wamepata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho, wajipange vilivyo na kufanyia kazi upungufu wote uliojitokeza kwenye mechi dhidi ya Zanaco," alisema Kaburu.
Achana na ya mtaani, haya hapa maneno kutoka uongozi wa Simba kuhusu Yanga kutolewa Ligi ya Mabingwa Achana na ya mtaani, haya hapa maneno kutoka uongozi wa Simba kuhusu Yanga kutolewa Ligi ya Mabingwa Reviewed by Steve on Wednesday, March 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.