Propellerads

Hali ya Ngoma na Tambwe ilivyo sasa, huenda kauli ya Daktari ikatoa hofu kwa mashabiki kuelekea mechi na Azam FC



Hii inaweza kua habari njema kwa mashabiki wa Yanga, kutokana na uongozi wao kusema kuwa wachezaji wao tegemeo, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wapo tayari kuanza mazoezi maalumu.

Wawili hao wamekuwa majeruhi ambapo walijikuta wakikosa baadhi ya mechi muhimu na sasa Daktari wa kikosi hicho, Edward Bavu, amesema wachezaji hao wameanza mazoezi mepesi kujiweka fiti, hivyo kutoa hofu iliyokuwa imetanda kwamba huenda wakakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC, Aprili mosi mwaka huu, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

"Ngoma na Tambwe wako katika hali nzuri na wamejiunga na wenzao kwa ajili ya mazoezi, masuala mengine tunaliachia benchi la ufundi ambalo lina dhamana ya upangaji wa kikosi chao," alisema Dk. Bavu.
Hali ya Ngoma na Tambwe ilivyo sasa, huenda kauli ya Daktari ikatoa hofu kwa mashabiki kuelekea mechi na Azam FC Hali ya Ngoma na Tambwe ilivyo sasa, huenda kauli ya Daktari ikatoa hofu kwa mashabiki kuelekea mechi na Azam FC Reviewed by Steve on Wednesday, March 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.