Propellerads

Kamati ya 'mauaji' mechi za kanda ya Ziwa yaundwa Simba SC, hatari hatari!!




Hakika unaweza kusema ni wazi sasa Simba imedhamiria kuchukua Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo juzi iliamua kuongeza kamati mpya ya kuhakikisha inavuna pointi tisa kwenye michezo mitatu inayotarajiwa kucheza Kanda ya Ziwa.

Ikiwa huko, Simba itacheza na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu mjini Bukoba kisha Toto African na Mbao FC mechi zote zitapigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya Simba, uongozi wa klabu chini ya Rais, Evans Aveva, umeteua kamati maalumu ya maangamizi ambayo itafanya juu chini kuhakikisha timu hiyo inavuna pointi tatu kwa kila mchezo watakaocheza.

"Jamaa wamejipanga kweli kama unakumbuka ile timu ya kina Julio (Jamhuri Kihwelo) iliyoundwa kwenda kule Songea kupambna na Majimaji, sasa imeongezewa watu wengine ambao wataenda kuweka kambi Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha wanavuna pointi zote tisa katika michezo watakayocheza huko." kilieleza chanzo.
Kamati ya 'mauaji' mechi za kanda ya Ziwa yaundwa Simba SC, hatari hatari!! Kamati ya 'mauaji' mechi za kanda ya Ziwa yaundwa Simba SC, hatari hatari!! Reviewed by Steve on Wednesday, March 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.