Niyonzima adokeza tena safari yake ya Cyprus, kwa sasa anasema hivi...
Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, ameweka bayana kwamba kama dili lake la kutua nchini Cyprus likitimia, atakuwa radhi kuihama timu yake hiyo ambayo amedumu nayo kwa miaka sita.
Niyonzima aliyesajiliwa Yanga akitokea APR ya kwao Rwanda, yupo mbioni kumaliza mkataba wake na klabu hiyo ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
"Kama mambo yakienda sawa kule Cyprus, basi nitaachana na Yanga kwa sababu sasa nahitaji timu ya kwenda kupata changamoto mpya baada ya kuwepo hapa kwa kipindi kirefu, hivyo ni muda wa kupisha watu wengine waje kuiendeleza timu hii.
"Nashukuru kwamba nimekuwepo kwa muda wote na nimechangia kwa ukubwa mafanikio ya timu hii kwa kipindi cha hivi karibuni, lakini nitaondoka ikiwezekana mwishoni mwa msimu huu kwa ajili ya kwenda kutangaza jina sehemu nyingine kama ambavyo nimefanya nilivyokuwa hapa," alisema Niyonzima.
Kwa sasa anaweza kuondoka mudawowote katika kikosi hicho kwa ajili ya kwenda kusaka zali la kukipiga nchini humo.
Niyonzima adokeza tena safari yake ya Cyprus, kwa sasa anasema hivi...
Reviewed by Steve
on
Wednesday, March 22, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment