Propellerads

Ukiachana na Kenny Ally, Yanga waanza mipango ya kukisuka kikosi kwa msimu ujao, Lwandamina kuleta wawili ndani...



Akiendelea kukiboresha kikosi chake, Kocha Mkuu wa Yanga Mzambia, amekabidhi majina mawili ya kiungo na mshambuliaji mmoja wa kimataifa atakaowasajili kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo tayari imeanza maandalizi ya usajili wa wachezaji wapya wa msimu ujao wa ligi kuu kwa kuanza kufanya mazungumzo na kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Lwandamina tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji wawili kwa uongozi ambao anaamini kama akiwapata kazi itakuwa imemalizika kutokana na ubora wa wachezaji hao.

Inadaiwa majina hayo amepanga kuyakabidhi mara baada ya kurejea nchini akitokea nyumbani kwao Zambia alikobaki baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa kumalizika dhidi ya Zanaco.

"Hatutaki kumuingilia kocha wetu kwenye usajili wake na kwa kifupi tulichopanga ni kumuachia kila kitu yeye kuamua mchezaji yupi amsajili na yupi amuache ili kuepuka visingizio baadae.

"Hivyo hivi karibuni tulifanya kikao na Lwandamina na akatuambia kuwa tayari amewaona wachezaji wawili wa kimataifa ambao anaamini kama wakiwapata, basi kikosi chake kitakuwa tishio.

"Majina hayo mawili amepanga kuyakabidhi kwa viongozi mara baada ya kurejea Dar akitokea Zambia alikobaki kwa ajili ya kuiangalia familia yake, tunaamini wachezaji hao ni wazuri kwa kuwa wanatoka kwenye hiyo na anawafahamu," kilieleza chanzo cha taarifa.
Ukiachana na Kenny Ally, Yanga waanza mipango ya kukisuka kikosi kwa msimu ujao, Lwandamina kuleta wawili ndani... Ukiachana na Kenny Ally, Yanga waanza mipango ya kukisuka kikosi kwa msimu ujao, Lwandamina kuleta wawili ndani... Reviewed by Steve on Wednesday, March 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.