Propellerads

Baada ya mechi na Madini FC, Simba wanamtaka kiungo huyu



Simba sio watu wa mchezo mchezo, kwani baada ya kuona uwezo mkubwa wa kiungo wa Madini FC ya jijini Arusha, Awesu Awesu, haraka sana wakatafuta mawasiliano naye, lengo likiwa kumalizana naye kabla wapinzani wao hawajazunguka mlango wa nyuma.

Kiungo huyo alifanya kazi kubwa katika nafasi yake kwenye mchezo huo, hali iliyopelekea Simba kushindwa kufanya mashambulizi kutokana na umahiri wake.

Kuwapo kwa mchezaji huyo kuliifanya Simba kushindwa kuonyesha kiwango kizuri na kuwafanya viungo wa Simba kutopata nafasi ya kufanya mashambulizi mpaka alipotolewa ndipo mwanya ukapatikana na hatimaye kupata nafasi ya kufunga bao la ushindi kupitia Laudit Mavugo.

Kitendo cha kufanya vizuri kwa kiungo huyo kimemshawishi Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, kumfuata na kuhitaji mawasiliano (namba ya simu) kwa ajili ya kuwa karibu.

Mchezaji huyo alipotafutwa alikiri ni kweli Hanspope alimfuata baada ya mechi kumalizika na kutaka namba yake,

"Ni kweli nilizungumza na huyo bosi, aliniambia nimpatie namba yangu ya simu kwa ajili ya kuwa karibu yangu, suala la kujiunga na Simba hajaniambia," alisema.
Baada ya mechi na Madini FC, Simba wanamtaka kiungo huyu Baada ya mechi na Madini FC, Simba wanamtaka kiungo huyu Reviewed by Steve on Tuesday, March 21, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.