Propellerads

Uwezekano wa Okwi kuja Msimbazi unazidi kupanda kila siku




Baada ya kufanikiwa kuiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uganda, klabu ya SC Villa kutokana na kufunga mabao muhimu, mshambuliaji Emmanuel Okwi ameendelea kuonyesha umwamba wake hata kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda 'Cranes'.

Okwi anahusishwa na mipango ya kurejea katika klabu ya Simba msimu ujao na tayari amefichua kwamba, hataongeza mkataba wake na SC Villa baada ya huu wa sasa wa miezi sita kumalizika.

Okwi aliifungia timu yake hiyo bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya kombaini ya majimbo, Mashariki mwa nchi hiyo, bao lake likitokana na mkwaju mkali wa faulo, hilo likiwa bao bao lake la nne tangu kutua nchini kwao akitokea SonderjyskE ya nchini Denmark.

Kwa sasa mshambuliaji huyo amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kutokana na uwezo wake mkubwa anaouonesha.
Uwezekano wa Okwi kuja Msimbazi unazidi kupanda kila siku Uwezekano wa Okwi kuja Msimbazi unazidi kupanda kila siku Reviewed by Steve on Tuesday, March 21, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.