Hii ni rekodi ya kipekee aliyoiweka Chirwa ligi kuu
Mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa ameweka
rekodi ya kipekee katika ligi kuu bara msimu huu baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi tatu ndani ya muda mfupi.
Chirwa alionyeshwa kadi hizo juzi Jumatano katika mchezo wa dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Taifa, ambapo Yanga walishinda kwa magoli 2-0.
Mwamuzi wa mechi hiyo, Ahmed Simba kutoka Kagera, alianza kumuonyesha Chirwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 44 kwa kubaini kua mshambuliaji huyo alimdanganya kufunga baao kwa kutumia mkono.
Mara baada ya kuonyeshwa jadi hiyo, Chirwa alionyeshwa kadi ya pili ya njano iliyoambatana na nyekundu dakika ya 45 baada ya kudundisha mpira kwa hasira wakati mwamuzi alipopuliza filimbi kuashiria mchezaji huyo alifanya faulo wakati anawania mpira na Nguya wa Ruvu.
Kwa muda ambao mwamuzi Ahmed Simba alioutumia kumuonyesha kadi hizo zote tatu Chirwa, ni sekunde 57 ambao ni mfupi kuwahi kutokea kwa mchezaji mmoja kuonyeshwa kadi tatu tangu msimu huu wa ligi kuu bara ulipoanza Agosti mwaka jana.
Hii ni rekodi ya kipekee aliyoiweka Chirwa ligi kuu
Reviewed by Steve
on
Friday, March 03, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, March 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment