Bossou aomba yaishe Yanga
Beki wa Yanga raia wa Togo ambaye hivi kribuni alikuwa katika
matatizo na uongozi wa klabu kwa mdai ya kutolipwa mishahara yake ya miezi minne, Vincent Bossou inaelezwa kuwa ameomba radhi ndio maana hata katika mchezo wa juzi dhidi ya Ruvu Shooting alicheza.
"Aliomba radhi baada ya kugundua kuwa alifanya makosa na uongozi ulimsamehe, ndiyo jana (juzi) alipangwa," kilisema chanzo.
Hata hivyo alipobanwa na mwandishi mwingine tena alisema "Kocha (Lwandamina) ndiyo sababu kubwa ya mimi kurejea uwanjani, alinihitaji kikosini na sikuona sababu ya kukataa. Nilikutana naye tukazungumza vizuri."
Alipotafutwa Bossou, alijibu kwa ufupi; "Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa ila kuhusiana na madai yangu bado sijalipwa."
Upande wa katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alipoulizwa alisema: "Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa nimetingwa na kazi nyingi naomba uniache mpaka kesho (leo)."
Bossou aomba yaishe Yanga
Reviewed by Steve
on
Friday, March 03, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, March 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment