Propellerads

Unajua Kichuya sasa hivi huko kwao Morogoro wanamchukuliaje!?, utapenda asee




Mshambuliaji huyo aligundua maisha yake yamebadilika baada ya kurejea kwao
Morogoro, mara tu baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba ambayo yeye alifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho na matokeo kuwa 1-1.

Kichuya kama kama mfalme, kwani hata madereva taxi na wale wa bodaboda hawataki malipo wanapomchukua.

Inaonekana watu wa Morogoro hata wasio mashabiki wa Simba wanajivunia kutokana na kazi nzuri anayoifanya.

Kichuya amekuwa na mafanikio makubwa katika mechi chache tu alizoichezea Simba kutokana na mchango wake mkubwa katika upachikaji mabao pamoja na kutoa pasi.

Hata hivyo, Kichuya amekuwa akisema kwamba hawezi kubweteka hata kidogo kutokana na namna watu wanayoonyesha kumjali badala yake ataongeza juhudi zaidi.

Unajua Kichuya sasa hivi huko kwao Morogoro wanamchukuliaje!?, utapenda asee Unajua Kichuya sasa hivi huko kwao Morogoro wanamchukuliaje!?, utapenda asee Reviewed by Steve on Tuesday, October 04, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.