Propellerads

Kuelekea Toto vs Simba leo, unaambiwa uwanjani ni full ulinzi tu kuhofia hujuma




Leo Jumamosi Toto Africans inaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini kitu kilichosisimua zaidi ni kwamba 'makomandoo' wa timu hizo wamekesha wakiulinda uwanja huo wakihofia vitendo vya ushirikina.

Imeelezwa kuwa, kila timu inaogopa kuhujumiwa na wapinzani wao hivyo wakajikuta wote wanalinda uwanja huo usiku wa kuamkia Ijumaa.

Mmoja wa walinzi wa uwanja huo alisema, makomandoo hao waliingia tangu juzi usiku wakitangulia wale wa Toto kisha wakaja wa Simba wakitaka kulinda uwanja.

"Walianza kuja watu wa Toto, baadaye kidogo wakaja Simba, sasa walivyoomba kulinda tukawafungulia na kama unavyowaona tupo nao hapa, tuliwaruhusu kwani timu zao zinakaribia kucheza," alisema mlinzi huyo.

Mechi ya Toto na Simba mara nyinhi huwa ngumu kwa miaka mitano Simba imeshindwa kuifunga timu hiyo uwanjani hapo na msimu uliopita zilipokutana zilitoka sare ya bao 1-1.

Kuelekea mchezo huo, Toto imeweka kambi katika Wilaya ya Ukerewe wakati Simba kwa siku tatu mfululizo imefanya mazoezi katika uwanja huo.
Kuelekea Toto vs Simba leo, unaambiwa uwanjani ni full ulinzi tu kuhofia hujuma Kuelekea Toto vs Simba leo, unaambiwa uwanjani ni full ulinzi tu kuhofia hujuma Reviewed by Steve on Saturday, April 15, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.