Yanga nao waamua kukomaa naa rufaa yao, wadai kutokuwa na imani na kamati
Baada ya Simba kushinda rufaa kwenye Kamati ya Masaa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kupewa pointi tatu, uongozi wa Yanga umepanga kwenda kwenye Kamati ya Nidhamu, Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa ajili ya kudai pointi.
Yanga imefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja tangu Simba washinde rufaa yao baada ya Kagera Sugar kumchezesha Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 Aprili 2, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera ikishinda kwa mabao 2-1.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona wapinzani wao Simba kushindwa kupata matokeo uwanjani na badala yake wanakimbilia za mezani.
Mkemi alisema, hawana imani tena na kamati hiyo ya Saa 72 na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ambayo yenyewe inatakiwa iwajibishwe kwa kushindwa kutunza kumbukumbu zao vizuri.
Alisema wameikumbusha Kamati ya Nidhamu ya TFF kupitia rufaa yao waliyoikata baada ya Lyon mchezaji Venance Ludovic mwenye leseni ya Mbao FC kwa ajili ya kupata pointi zao tatu.
"Wenzetu Simba tunaona kabisa ushindi wa uwanjani umewashinda wanang'ang'aniza ushindi wa mezani, hivyo basi na sisi tumeona tutumie njia hiyo wanayotumia tupate pointi tatu.
"Hivyo, tumepanga kwenda TFF kwa ajili ya kukumbushia rufaa yetu tuliyomkatia mchezaji Ludovic aliyeichezea Lyon akiwa na leseni ya Mbao aliyokuwa anaichezea na hilo lipo wazi kabisa mchezaji huyo amesimamishwa na shirikisho hilo kwa muda baada ya kubaini kuna makosa.
"Niongeze kwa kusema kuwa, Yanga hivi sasa hatuna imani na kamati ya Saa 72 inayoongozwa na mashabiki wengi wanazi wa Simba ambao wameshiriki kuipa pointi za chee Simba," alisema Mkemi.
Yanga nao waamua kukomaa naa rufaa yao, wadai kutokuwa na imani na kamati
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment