Baada ya maamuzi ya Kamati, Maxime atoa msimamo wake, Fakhi naye aongea
Siku moja baada ya kupokwa pointi tatu, Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema anaamini mchezaji wake Mohammed Fakhi ana kadi mbili tu za njano tofauti na ilivyoamuliwa na Kamati ya Saa 72.
Juzi Alhamisi usiku, Simba ilipewa pointi tatu na mabao matatu na Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kosa la Kagera Sugar kumchezesha Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Katika mchezo huo uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba.
Maxime amesema kuwa hatua hiyo ni uonevu kwani yeye na viongozi wake wanaamini Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na siyo tatu kama ilivyodaiwa.
"Ninavyojua Fakhi ana kadi mbili tu siyo tatu, ila kwa kuwa uamuzi umeshafikiwa sina la kufanya n kuhusu suala zima la kutafuta haki yetu nauachia uongozi wa Kagera Sugar.
"Simba wasishangilie pointi walizopata kwani ligi bado haijamalizika na naamini lolote linaweza kutokea dhidi yao.", alisema Maxime.
Kwa upande wake, Fakhi alisema "Mimi sielewi lolote hadi sasa kwani nina kadi mbili tu za njano, naona Simba wanatafutiwa ubingwa kwa nguvu, huu ni uonevu kwa timu nyingine."
Baada ya maamuzi ya Kamati, Maxime atoa msimamo wake, Fakhi naye aongea
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment