Kuelekea mchezo na Simba, Toto waonesha hofu kwa mwamuzi kutokana na sababu hii
Kesho Jumamosi kikosi cha Simba kitashuka kwa mara nyingine kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kupambana na Toto Africans baada ya Jumatatu iliyopita kuitembezea kichapo Mbao FC kwa mabao 3-2.
Hata hivyo, mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo amezua balaa jijini humo baada ya uongozi wa Toto Africans kudai kuwa hauna imani naye.
Mmoja wa viongozi wa Toto ambaye aliomba kutotajwa jina lake, ameffunguka kuwa mwamzui Jacob Adongo ambaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimpatia onyo kali baada ya kushindwa kutafsiri vizuri sheria katika mechi ya Simba dhidi ya Mbeya City, ndiye amepangwa kuchezesha mechi yao.
Alisema kutokana na hali hiyo hawana imani naye kwani wanahofia kuwa yale aliyoyafanya katika mechi ya Simba na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa Dar anaweza kuyafanya tena dhidi yao.
"Kusema kweli hatuna imani naye na tayari tumeshawaambia TFF kuhusiana na hilo," alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama, alisema: "Kila mwamuzi anayechezesha ligi tunamuamini, sioni haja ya wao kulalamika."
Kuelekea mchezo na Simba, Toto waonesha hofu kwa mwamuzi kutokana na sababu hii
Reviewed by Steve
on
Friday, April 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment