Propellerads

Yanga katika mazungumzo na kiungo huyu wa Azam atakayesaidiana na kina Zulu, Makapu




Yanga iliyo chini ya Kocha George Lwandamina, raia wa Zambia, ipo kwenye mazungumzo ya awali kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa Azam FC, Mudathir Yahya.

Kiungo huyo wakati timu hiyo inanolewa na Mholanzi, Hans Pluijm msimu wa 2014/2015, aliwahi kupendekezwa kwenye usajili wake akiwemo pia winga, Farid Mussa anayecheza soka la kulipwa nchini Hispania lakini mambo yakashindikana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Yanga imeelekeza nguvu tena kwa Mudathir kuhakikisha wanampata kwa ajili ya kuiimarisha safu yao ya kiungo. Mudathir amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha Azam katika siku za hivi karibuni.

Mmmoja wa watu muhimu katika Kamati ya Mashindano ya Yanga, alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha wanatumia ushawishi wote ili kuhakikisha wanamsajili Mudathir ili asaidiane na Justine Zulu na Juma Makapu.

Alipotafutwa Meneja Mkuu wa Azam, Philipo Allando kuzungumzia hilo, alisema huu siyo muda wa kuzungumzia hilo, wakati Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema: "Nipo Morogoro nimepatwa na msiba, hivyo sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo."
Yanga katika mazungumzo na kiungo huyu wa Azam atakayesaidiana na kina Zulu, Makapu Yanga katika mazungumzo na kiungo huyu wa Azam atakayesaidiana na kina Zulu, Makapu Reviewed by Steve on Monday, April 10, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.