Kigogo Azam awashangaa Simba juu ya Manyika, awapa ushauri huu
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ameshangazwa na kitendo cha mlinda mlango chipukizi wa Simba, Peter Manyika kuendelea kukaa benchi kikosini hapo huku akiwashuhudia wageni wakija na kuchukua nafasi yake.
Kwa muda mrefu, Manyika amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba mbele ya makipa wa kigeni, ambapo awali alikuwa akiwekwa benchi na Muivory Coast, Vincent Angban kabla hajafungashiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Mghana, Daniel Agyei.
Akizungumzia ishu hiyo, Kawemba amesema: "Tunatakiwa kuwapa nafasi vijana wetu ili waje kuwa na faida kwenye timu yetu ya taifa, sasa nashangaa kwa nini Manyika amekuwa akiwekwa benchi kwa muda mrefu ndani ya Simba.
"Manyika kwa umri wake ulivyo unaendana na kipa wetu Aishi Manula, sasa huu ndiyo ulikuwa muda muafaka kwake kucheza kwa ajili ya kulisaidia taifa, tayari tumeiunda timu ya Serengeti Boys ambayo inaonekana kuwa imara, sasa tunapaswa pia kuandaa timu ya vijana ya chini ya miaka 23 ambayo wachezaji wake ndiyo hawa kina Manyik."
Kigogo Azam awashangaa Simba juu ya Manyika, awapa ushauri huu
Reviewed by Steve
on
Monday, April 10, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment