Kufuatia kuhusishwa na madai ya rushwa, Mourinho amejitetea
Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho ambaye ni
miongoni mwa mameneja waliotuhumiwa kujihusisha na malipo yasiyokua halali, sasa amefunguka kuhusu uvumi huo.
Aliyekua kocha wa England, Sam Allardyce alipoteza kibarua chake baada ya taarifa za kushtukiza zikimhusisha yeye na mipango ya rushwa.
Pia ilidaiwa kwamba makocha nane waliopita na wengine wapo Premier League walipokea malipo isivyo halali kutoka kwa mawakala ili kusaidia kupindisha bei za usajili wa wachezaji huku Mourinho akidaiwa kua miongoni.
"Kitu nisichopendelea- kiukweli ninachukia na siwezi kubali, ni tetesi," alisema kama alivyonukuliwa na Daily Star.
"Huwezi kufurahia tetesi na hii inatokana sana na kusikiliza tetesi.
"Unamtuhumu mtu, ndio, dunia nzima inajua na hutakiwi kuficha chochote.
"Lakini tetsi sio nzuri. Mashaka sio vizuri. Ndio kitu pekee ninachoweza kusema."
Kufuatia kuhusishwa na madai ya rushwa, Mourinho amejitetea
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 04, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 04, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment