Barua ya Yanga wakiomba kutumia uwanja wa Amaan
Uongozi wa klabu ya Yanga, umeandika barua kuomba kuutumia
Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.
Yanga imechukua uamuzi huo baada ya Serikali kutangaza kuifungia yenyewe pamoja na Simba kuutumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Serikali imetangaza kuufungia uwanja huo baada ya vurugu za mashabiki zilizojitokeza wakati wa mechi ya watani hao.
Uamuzi huo wa Yanga kama utapita kupitia ombi lao, maana yake timu zitalazimika kusafiri kwenda Zanzibar kuifuata Yanga ambayo itakuwa nyumbani.
Barua ya Yanga wakiomba kutumia uwanja wa Amaan
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 04, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, October 04, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment