Kuhusu kadi nyekundu ya Xhaka, Wenger ametoa mtazamo wake na hatua itakayochukuliwa
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu
haitakata rufaa yoyote kuhusu maamuzi yaliyofanyika kumtoa nje Granit Xhaka kwenye mechi ya Premier League dhidi ya Swansea City.
Gunners wameshinda mechi sita mfululizo baada ya kuwazamisha Swansea jana kwa 3-2 lakini hata hivyo walijikut wakicheza wakiwa 10 pekee dakika 20 za mwishoni baada ya Xhaka kupewa kadi nyekundu baada ya kukumbana na Modou Barrow.
Wenger anaamini maamuzi ya Jonathan Moss makubwa mno kwa tukio lile, lakini amefunguka kwamba hatakata rufaa kutokana na aina ya kosa lenyewe.
"Hapana (Hatutakata rufaa kwa maamuzi) ni maamuzi makubwa mno, faulo ilikua wazi ni ya makusudi. Ilionekana kama kadi ya njano lakini mwamuzi kaamua kutoa nyekundu." Wenger aliwaambia waandishi.
Kuhusu kadi nyekundu ya Xhaka, Wenger ametoa mtazamo wake na hatua itakayochukuliwa
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 16, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 16, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment