Wenger atoa mtazamo wake kuhusu penati iliyowapatia ushindi kwa Southampton
Arsene Wenger amekataa kuzungumzia maamuzi ya mwamuzi Robert Madley
kuwapatia Arsenal penati ya mwishoni jana wakipambana na Southampton.
Mechi hiyo iling'ang'ania kwa sare ya 1-1 mpaka muda wa majeruhi mpaka pale mwamuzi alipotoa penati baada ya Olivier Giroud kuchezewa vibaya na Jose Fonte.
Fonte alivuta jezi ya Giroud wakati akiwa na mpir katika eneo la hatari la Southampton, ambapo Santi Cazorla alipiga mkwaju huo na kuwapatia Arsenal pointi tatu muhimu.
Mwamuzi Madley alionekana kufanya maamuzi sahihi kwa kutoa penati, ingawa mtangazaji mmoja wa TV wa Sky Sports hakukubaliana na maamuzi hayo.
Wengel alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusu tukio lile kwa sababu hakuona 'replay' yake, lakini alifunguka ndio sababu kubwa ya timu yake kupanta point tatu.
"Ki ukweli kila mtu ananiambia ilikua ni penati, lakini sikuweza kuona tena." alisema Wenger.
Wenger atoa mtazamo wake kuhusu penati iliyowapatia ushindi kwa Southampton
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 11, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 11, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment