Huyu hapa Theo Walcott akizungumzia mchezo wa jana, atoa sababu za kushindwa
Theo Walcott amesisitiza kua matokeo ya kufungwa jana na Dinamo Zagreb
hayana athari yoyote kwa maandalizi yao dhidi ya Chelsea jumamosi.
The Gunners walianza kampeni yao ya UEFA kwa matokeo mabovu jana usiku ambapo ilishuhudiwa Olivier Giroud akitolewa nje baada ya kadi mbili za njano.
"Kawaida ni vigumu sana kama mkicheza watu kumi pekee" alisema Walcott.
"Tuna uzoefu wa kucheza watu kumi lakini ilituwia vigumu sana. Kusema ukweli hatukufikiria kama tungejikuta tunacheza kumi pekee.
"Tulicheza vizuri zaidi kipindi cha pili, tulimiliki mpira zaidi.
"Lakini tulichelewa, tunatakiwa kusonga mbele kwa sasa . Tuna mchezo mkali, muhimu, weekend hii lakini kila mmoja atakua dissapointed.
Walcott ambaye aliingia akitokea bench na kuifungia Gunners jana, anaamini kupoteza kwao sio kikwazo kwao kushinda Ulaya msimu huu.
"Hatuwezi kukatishwa na mechi moja na kusema ndio mwisho."
"Bado tuna safari ndefu klabu bingwa, tulikuwa na vikwazo vingi kabla lakini tumevivuka vyote.
"Tumekua kwenye hii michuano kwa miaka 18 sasa kwa hiyo tua uzoefu mkubwa na tunajua namna ya kupambana na vikwazo . Tunatakiwa kurudi na nguvu zaidi.
Mechi hiyo ya jana katika michuano ya klabu bingwa Ulaya ilishuhudiwa Arsenal akipoteza ugenini kwa 2-1 mbele ya Dinamo Zagreb ya nchini Croatia.
Huyu hapa Theo Walcott akizungumzia mchezo wa jana, atoa sababu za kushindwa
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 17, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment