Propellerads

Willian na Pedro kuikosa Arsenal, Mourinho athibitisha



Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amethibitisha kua nyota
wake wawili, Willian na Pedro hawatakuwemo kwenye kikosi kitakachocheza na Arsenal jumamosi Stamford Bridge.

Pedro hakuemo kwenye kikosi kilichoshinda 4-0  dhidi ya Macab Tel Aviv kwenye klabu bingwa jana usiku kutokana na majeraha huku Willian ambaye alifunga bao la kwanza alitolewa kutokana na tatizo la misuli.

"Willian kweli yupo nje. Nadhani na Pedro nae yupo nje. Napenda zaidi pale wachezaji wanapoumia wakicheza vizuri kuliko kuumia wakati wanacheza vibaya." Mourinho aliwaambia waandishi baada ya mchezo kumalizika.

Mabingwa hao wa Premier League wameshinda mchezo mmoja pekee kati ya mitano waliyocheza huku wakiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi.
Willian na Pedro kuikosa Arsenal, Mourinho athibitisha Willian na Pedro kuikosa Arsenal, Mourinho athibitisha Reviewed by Steve on Thursday, September 17, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.