Kauli ya Wenger kufuatia kupoteza kwa Dinamo Zagreb
Jana usiku kwenye mechi ya UEFA ambapo vijana wa Arsene Wenger
walilala mbele ya Dinamo Zagreb, kuna mambo mengi yanazungumziwa hivi sasa. Lawama kwa Wenger ni kawaida kutoka mashabiki na wadau wa club hiyo lakini na yeye pia hakosagi cha kusema.
Baada ya mechi Wenger hakufurahishwa na kadi nyekundu kwa Giroud na alisema hivi,“Tulikua hatuna bahati kidogo usiku wa leo, naamini goli la kwanza lilikua offside. Hatukua kwenye ubora wetu lakini pia refa hakua kwenye ubora wake. Kadi ya kwanza kwa Giroud ni kosa lake mwenyewe Giroud. Lakini kadi ya pili hapana, amekua na bahati mbaya kumgusa mchezaji kwasababu hakumuona yule mchezaji na ilikua bahati mbaya kabisa lakini imetokea. Simuelewi refa, kama ingekua makusudi sawa lakini haikua hivyo”
“Kama usiposhinda game inabidi uangalie wapi ulienda wrong, lakini sioni kama wachezaji wamecheza vibaya, wamejitaidi lakini mambo hayakua kwetu leo"
Kauli ya Wenger kufuatia kupoteza kwa Dinamo Zagreb
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 17, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment