Propellerads

Rafu za Prisons zamshitua Pluijm, aonesha hofu yake




Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema itakuwa ni
hatari sana kama waamuzi watakaa kimya uchezaji wa kibabe wenye kulenga kuwaumiza wachezaji wa timu maarufu au kubwa.

Pluijm amesema, wachezaji wa Prisons walionekana wazi kuzidiwa kiushindani walipocheza nao na walilenga kuumiza wachezaji wa Yanga.

“Hazikuwa faulo za kimpira, walikuwa watu waliolenga kuwaumiza wachezaji wangu. Ni kitu kibaya kabisa na haiwezi kuwa sahihi,” alisema Pluijm.

“Hakuna soka bila faulo, lakini faulo ya kisoka na faulo iliyo nje ya soka zinatofautiana pia ni vitu vinavyoonekana wazi.”

Kocha huyo Mholanzi alisema kuna kila sababu ya waamuzi kukaa chini na kulijadili suala hilo.

Ikiwezekana wachezaji walindwe na kuwe na adhabu kali kuwakumbusha wale wanaolenga kuumiza wengine kwa makusudi.

Undava wa Prisons huku ikipoteza kwa bao 3-0 dhidi ya Yanga, ulisababisha Pluijm kuzozana na mwamuzi wa mechi hiyo.

Rafu za Prisons zamshitua Pluijm, aonesha hofu yake Rafu za Prisons zamshitua Pluijm, aonesha hofu yake Reviewed by Steve on Friday, September 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.