Baada ya kupoteza kwa Man City, Mourinho aelekezea lawama zake huku
Jose Mourinho amemtupia lawama mwamuzi Mark Clattenburg kwa kufanya
makosa baada ya kushindwa kuwapa penati hata moja katika mechi ya jana Jumamosi waliyopoteza kwa 2-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City.
United wangeweza kupata penati mbili ambazo mwamuzi alizikaushia baada ya mlinda mlango Claudio Bravo kumchezea rafu Wayne Rooney ndani ya eneo la hatari, huku Nicolas Otamendi alizuia mpira kwa bega kuzuia krosi iliyotoka kulia.
Akizungumza baada ya mechi, Mourinho aliyejaa ghadhabu aliiambia Sky Sports News "Tuliadhibiwa na Mark kwa maamuzi yake mabaya kipindi cha pili. Ninajua sheria za mchezo. Ni wazi ilikua ni penati na kadi nyekundu kwa Bravo.
"Kama ni nje ya boksi, ni faulo ya moja kwa moja na kadi nyekundu. Ndani ya boksi inatakiwa iwe hivyo hivyo. Hata makocha wazuri wanaweza kufanya makosa, na yeye amefnya kubwa. Iliwezekana kua 2-2 mapema tu, na tungekua tunazungumzia stori nyingine kabisa.
"Penati ya pili ilikua ni ya Otamendi. Wengi mtasema sio penati. Asilimia 100 ninasema Otamendi alizuia krosi ya goli lakini ilikuja nyuma yake, alijua ndio maana alirudisha nyuma mkono mwingine. Penati kabisa."
Mechi ya jana ilikua ni ya kwanza kupoteza kwa Man United msimu huu pia ya kwanza katika mechi nne zilizopita vilabu hivyo vikikutana.
Baada ya kupoteza kwa Man City, Mourinho aelekezea lawama zake huku
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 11, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 11, 2016
Rating:



No comments:
Post a Comment