Ronaldinho kurejea tena Barca
Mkongwe wa FC Barcelona, Ronaldinho ni mchezaji huru na sasa amehusishwa
na klabu yake hiyo ya zamani kwa mara nyingine.
Nyota huyo ambaye alitumikia miaka mitano Camp Nou, hana klabu tangu aondoke Fluminense Septemba 2015.
Hata hivyo, amehusishwa tena na Barca ili kuitangaza klabu hiyo ya Catalan nchini Marekani.
Barca watafungua ofisi mpya New York ifikapo Septemba 6 na Ronaldinho atakua kama balozi wa klabu katika sherehe za ufunguzi.
— FC Barcelona (@FCBarcelona) September 2, 2016Katika mpango huo rais Josep Maria Bartomeu na wana bodi wengine wataelekea Marekani ili kuendesha miradi mbali mbali ya kijamii na ya kujitolea ili kupanua umaarufu wa klabu kufikia soko la America.
Ronaldinho kurejea tena Barca
Reviewed by Steve
on
Monday, September 05, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 05, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment