Kikosi cha Yanga kinachosafiri kesho kuumana na Ndanda
Kikosi cha wachezaji 20 wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC kinatarajiwa
kuondoka kesho asubuhi Dar es Salaam kwa basi kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Jumatano.
Hata hivyo, kikosi hicho cha Mholanzi, Hans van der Pluijm kitawakosa wachezaji wake tegemeo sita, ambao wana udhuru tofauti.
Hao ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ ambaye yupo kwenye msiba wa baba yake, mabeki Vincent Bossou ambaye yupona timu yake ya taifa ya Togo, Pato Ngonyani majeruhi sawa na winga Geofrey Mwashuiya.
Wengine ni kiungo Haruna Niyonzima ambaye yupo na timu yake ya taifa ya Rwanda na mshambuliaji Malimi Busungu ambaye pia ni majeruhi.
Kikosi kinachotarajiwa kusafiri kesho ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Beno Kakolanya, mabeki Juma Abdul, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Yussuf Mhilu wakati washambuliaji ni Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Kikosi cha Yanga kinachosafiri kesho kuumana na Ndanda
Reviewed by Steve
on
Monday, September 05, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 05, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment