Licha ya kua mchezaji bora Ulaya, hii ndiyo thamani ya Cristiano Ronaldo kwa sasa
Supa staa Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji 10 wa Real Madrid ambao
thamani yao imepungua tangu msimu uliopita.
Kwa mujibu wa Transfermarket, kikosi cha Zinedine Zidane kwa ujumla thamani yake imeongezeka tngu kuanza kwa msimu uliopita mpaka sasa, lakini kuna baadhi ya wachezaji ambao thamani yao imeshuka. Nyota mreno Ronaldo ni miongoni mwa nyota hao akiporomoka kwa 9% ikifananishwa na mwaka jana, huku kapteni Sergio Ramos naye thamani yake ikishuka pia.
Kinda Mhispania Marco Asensio amepanda mpaka kufikia 242% baada ya kuingia kikosi cha kwanza msimu huu ambapo pia Gareth Bale akiwa miongoni mwa waliopanda thamani msimu huu.
Hii hapa orodha ya wachezaji kumi walioporomoka thamani Real Madrid kutoka mwaka jana kwa mujibu wa Transfermarket.
Cristiano Ronaldo – kutoka €120m hadi €110m (ameshukaa 9% )
Mateo Kovacic – kutoka €22m hadi €20m (ameshuka 10% )
Danilo – kutoka €20m hadi €18m (ameshuka 10% )
Luka Modric – kutoka €55m hadi €50m (ameshuka 10% )
Sergio Ramos – kutoka €45m hadi €40m (ameshuka 11% )
Nacho – kutoka €6m hadi €5m (ameshuka 17%)
Kiko Casilla – kutoka €7.5m hadi €6m (ameshuka 20%)
Isco – kutoka €45m hadi €35m (ameshuka 23%)
Fabio Coentrao – kutoka €18m hadi €10m (ameshuka 45%)
Pepe – kutoka €15m hadi €6m (ameshuka 60%)
Licha ya kua mchezaji bora Ulaya, hii ndiyo thamani ya Cristiano Ronaldo kwa sasa
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 08, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 08, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment