Propellerads

'Kwanini Pogba na Mkhitaryan hawafanyi vizuri Manchester United'



Wachezaji wa Manchester United waliosajiliwa msimu huu
 Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan hawajacheza kwa viwango kama ilivyotarajiwa na wengi Old Trafford lakini wakala wao anadai anajua kwanini hawako vizuri kwa sasa.

Pogba alisajiliwa kutoka Juventus kwa pesa iliyovunja rekodi ya pauni mil 89, huku Mkhitaryan akinunuliwa kutoka Bundesliga klabu ya Borussia Dortmund.

Wakala wa wawili hao, Mino Raiola amefunguka kwamba Pogba hayupo sawa lakini ana imani atarejea kiwango chake muda si mrefu.

"Ni kweli Pogba hachezi vizuri kwa sasa, anachukua muda kuzoea na watu daima wanatarajia kuona makubwa," alisema kwa mujibu wa Daily Mail.

"Atatawala kwa miaka 10. Ni mtoto wa man United aliyepotea."

Kwa upande wa Mkhitaryan, Raiola anaamini pia naye atarejea kwenye kiwango chake.

"Mkhi alikua mchezaji bora kwenye ligi ya Ujerumani misimu miwili iliyopita."
'Kwanini Pogba na Mkhitaryan hawafanyi vizuri Manchester United' 'Kwanini Pogba na Mkhitaryan hawafanyi vizuri Manchester United' Reviewed by Steve on Tuesday, September 20, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.