Propellerads

Kuna mchezaji mmoja wa Manchester United 'amemmaindi' Mourinho kwa hiki alichomfanyia




Mmoja wa wachezaji kikosi cha Manchester United anadaiwa
kuchukizwa na kocha Jose Mourinho baada ya kukosolewa na Mreno huyo.

United walijikuta wakipoteza mchezo wa tatu mfululizo baada ya kushuhudia wakipigika kwa 3-1 mbele ya Watford Jumapili.

Mourinho hakuvutiwa na kiwango cha Luke Shaw kwenye mechi iliyopita huku akimkosoa hadharani beki huyo kwa kuzembea goli la pili la Watford.

Beki huyo wa kushoto ambaye atakosa wiki tatu uwanjani kutokana na majeraha amedaiwa kutofurahishwa na kitendo cha kocha wake.

Kwa mujibu wa The Times, Shaw anahisi ingekua bora zaidi kupewa maelekezo binafsi kutoka kwa kocha kuliko kulaumiwa hadharani..

Hii sio mara ya kwanza kwa Mourinho kuwakosoa wachezaji wake hadharani, ameshafanya hivyo kwa Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard baada ya mechi na Man City.
Kuna mchezaji mmoja wa Manchester United 'amemmaindi' Mourinho kwa hiki alichomfanyia Kuna mchezaji mmoja wa Manchester United 'amemmaindi'  Mourinho kwa hiki alichomfanyia Reviewed by Steve on Tuesday, September 20, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.