Huenda Giroud akakosa mechi ya Chelsea, lakini huyu mwingine hatocheza kabisa
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kwamba Olivier Giroud
anaweza kukosa mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Chelsea huku Aaron Ramsey akikosa kabisa kutokana na majeraha kwenye nyama ya paja.
Giroud ambaye alipewa kadi nyekundu wiki iliyopita kwenye mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Paris Saint-Germain, anasumbuliwa maumivu kwenye kidole.
Wenger ameiambia tovuti rasmi ya klabu ya Arsenal kwamba atasubiri mpaka mwishoni mwa wiki kuangalia uwezekano wa Giroud kuwemo mchezo na Chelsea uwanja wa Emirates.
Huenda Giroud akakosa mechi ya Chelsea, lakini huyu mwingine hatocheza kabisa
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 21, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 21, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment