Propellerads

Kwa mnaomkosoa Rooney amewapa jibu hili




Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ameweka wazi kwamba anapokea maneno kutoka kwa wanaomkosoa kama upuuzi tu.

Nyota huyo amekua katika kitimoto baada ya kua katika kiwango kinachosua sua msimu huu.

Rooney alicheza kama mshambuliaji kwenye mechi waliyoshinda kwa 3-1 dhidi ya Northampton Town kwenye EFL Cup huku akipigagolini shuti moja pekee.

Matokeo hayo yalitoa 'nuksi' ya kufungwa mechi tatu mfululizo kwa klabu hiyo, na Rooney anaamini kikosi kitakua bora zaidi kuanzia sasa.

"Huo ndio mpira nafikiri," Rooney aliiambia MUTV "Hatujashinda michezo mitatu, na bila shaka kila mtu atazungumzia hili. Tulikua na wiki mbaya.

"Nafikiri nimekosolewa sana katika kipindi changu chote, nadhani, lakini huo ndio mpira. Ninasikiliza makocha wangu na wana timu waenzangu, watu wote wanaonizunguka. Sisikilizi watu wengine wanasema nini kwa sababu ni mengi ni upuuzi."

"Ninatakiwa kua makini, kujituma, na bila shaka nimeshafanya wakati wangu wote. Nimefanya kazi na kujituma kwa timu yangu."
Kwa mnaomkosoa Rooney amewapa jibu hili Kwa mnaomkosoa Rooney amewapa jibu hili Reviewed by Steve on Friday, September 23, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.