Guardiola anamtaka nyota huyu kutoka Arsenal
Bosi wa Manchester City, Pep Guardiola ameripotiwa kutaka
kumleta nyota kutoka klabu ya Arsenal.
Kwa mujibu wa Daily Express, kocha huyo wa zamani wa FC Barcelona anataka kumchukua mshambuliaji Alexis Sanchez.
Inaaminika wazi kwamba nyota huyo wa Chile yupo katika mipango ya kukutana na uongozi wa klabu yake ya sasa Arsenal kuhusu mkatba mpya, lakini vilabu vingine vya Premier League vinapigia mahesabu ya kumnasa.
Tetesi zinadai kwamba mshambuliaji huyo anatarajiwa kua mchezaji anayelipwa zaidi Emirates ambapo anataka mkataba wenye thamani ya pauni 200 000 kwa wiki.
Guardiola anaangalia namna ya kuboresha nafasi ya ushambuliaji katika miezi kadhaa ijayo na anaamini Sanchez anamfaa zaidi.
Guardiola anamtaka nyota huyu kutoka Arsenal
Reviewed by Steve
on
Friday, September 23, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 23, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment