Omog amekazia Simba watamaliza mchezo mapemaa, Yanga mpoo!!
Siku zikiwa zinasonga kwa kasi kuelekea mechi dhidi ya Yanga, Kocha
Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema anataka kuona washambuliaji wake wanatumia kila nafasi watakayoipata ndani na nje ya 18.
Kuelekea mchezo wa Simba na Yanga nani atatoboa!!
Timu hizo kongwe, zinatarajiwa kuvaana Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mrundi, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib, Frederick Blagnon huku wakisaidiwa na kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya.
Omog alisema tayari ameshawaambia wachezaji wake katika hilo, kikubwa anataka kuona timu hiyo inatoka uwanjani ikiwa na ushindi wa aina yoyote.
Omog amesema tayari amewapa mbinu mbalimbali za ufungaji wa mabao kwa njia ya mashuti nje na ndani ya 18, kumchambua kipa na kutumia vema mipira ya krosi na kona kwa ajili ya kupiga vichwa.
“Nitakuwa mkali kwa yule mshambuliaji atakayeleta masihara ya kushindwa kutumia kila nafasi tutakayoipata ndani ya uwanja kwa ajili ya kufunga mabao.
“Kama unavyojua, siku zote bahati haiji mara mbili, hivyo basi ni vema washambuliaji wangu wakaongeza umakini kwa kuitumia vema kila nafasi tutakayoipata tutakapokutana na Simba na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu.
“Kikubwa nitaka niendelee kukaa kileleni hadi mwisho mwa ligi kuu ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa wa ligi kuu, ninavyojua siyo kazi rahisi, lakini tutapambana ili tufanikishe malengo yetu,” alisema Omog.
Omog amekazia Simba watamaliza mchezo mapemaa, Yanga mpoo!!
Reviewed by Steve
on
Friday, September 23, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 23, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment