Wenger ammwagia misifa Xhaka, amfananisha na mkongwe huyu
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amemsifia nyota mpya
waliyemsajili msimu huu Granit Xhaka kufuatia perfomance yake kwenye mechi ya jumamosi waliposhinda kwa 3-1 mbee ya Watford.
"Yupo vizuri, anaanza vizuri, ana balance katika mchezo wake, ana pasi fupi nzuri na pia ndefu. Ana miaka 24 tayari ana uzoefu ligi mbali mbali hili hua linakua tatizo endapo mchezaji ameshacheza kwingine. Ameshakua kapteni katika wakati wake Monchengladbach, hiyo sio klabu ndogo kwa hiyo ana uzoefu wa uongozi" Wenger aliwaambia waandishi.
"Ni mtu ambaye anacheza vizuri nyuma ya mpira. Kidogo amefanana na Petit jinsi anavyocheza "
Wenger ammwagia misifa Xhaka, amfananisha na mkongwe huyu
Reviewed by Steve
on
Monday, August 29, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 29, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment