Propellerads

Utaipenda hiki kituko!!, Mourinho atuhumiwa kuiba koleo



Bosi wa Manchester United ametuhumiwa kuiba koleo wakati wajenzi
wakiendelea na kazi kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo Carrington.

Wajenzi wapo katika eneo hilo kuongezea uwazi wa eneo hilo kama walivyoagizwa na mtangulizi wa Mourinho, Louis van Gaal wanafikiria kwamba walimkasirisha Mourinho baada ya kutumia vifaa vya mazoezi klabuni kama vile koni katika kazi zao.

Mourinho anaonekana kuingia matatani kutokana na kauli yake kwa wajenzi kwamba "Kama mkichukua vitu vyangu. Nitachukua na vya kwenu"

Chanzo kimoja kiliiambia The Sun kwamba "Ujenzi unasababisha msuguano na Mourinho kutokana na kuongezeka idadi ya watu ukilinganisha na eneo. Alienda kwenye eneo la ujenzi na kuwaambia 'acheni kuchukua vitu vyangu'."

Hata hivyo Manchester United hawajaongea chochote kuhusu mkasa huo.
Utaipenda hiki kituko!!, Mourinho atuhumiwa kuiba koleo Utaipenda hiki kituko!!, Mourinho atuhumiwa kuiba koleo Reviewed by Steve on Sunday, August 28, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.