Majabvi aongelea hatma ya mkataba wake na Simba
Kiungo Mzimbawe wa Simba, Justice Majabvi amesema kwa sasa
hana ndoto ya kuongeza mkataba hata kama atatakiwa kufanya hivyo, badala yake anasubiri kwanza mpaka huu wa kwanza umalizike ili ajipime kama kweli anaweza kuendelea kucheza soka la Bongo.
Kiungo huyo mwenye miaka 31, ametaja sababu kuu kuwa ni umri wake kuwa mkubwa kwa ngazi ya kimataifa, hivyo asingependa kuharibu CV yake, kama atakimbilia kusaini mkataba mwingine wakati umri umekwenda, kwani huko mbele wanaweza kumtema jambo ambalo anasema litachafua wasifu wake wa kazi.
“Kuongeza mkataba! Kwa sasa sina ndoto hiyo nasubiri huu wa kwanza uishie kisha nitajipima kama ninaweza kuendelea ama la.
“Ujue sifa kuu ya mchezaji wa kimataifa, ni lazima awe na kiwango cha kuweza kuisaidia timu, sasa kwa umri wangu ni lazima niangalie mwishoni kama kweli uwezo wa kuendelea kucheza ninao ama la, siyo kukimbilia kuongeza mkataba kisha unajiharibia CV yako kwa kutemwa. Sitaki kujichafulia CV yangu,” alisema Majabvi.
Kiungo huyo alisaini mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo na hivyo mwakani atatakiwa kusaini mkataba mpya na timu hiyo au atakuwa huru kuondoka zake.
Majabvi aongelea hatma ya mkataba wake na Simba
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment