Kuhusu kutimuliwa Chelsea Mourinho asema yake

Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amesema kamwe hatakimbia
Stamford Bridge eti kisa kile kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Southampton.
Lakini akasisitiza, kama wanataka kumfukuza, poa tu lakini watajuta kumfukuza kocha gwiji ambaye hawakuwahi kuwa naye.
Mourinho ameiambia runinga ya Sky hivi: “Moja, kamwe siwezi kukimbia, siwezi kukimbia majukumu yangu.”
“Pili kama klabu wanataka kunitimua, basi wafanye hivyo lakini watajuta kumfukuza kocha bora kama mimi.”
Licha ya kutangulia kufunga, Chelsea ikiwa nyumbani imekutana na kipigo hicho cha mabao 3-1 dhidi ya Southampton.
Kuhusu kutimuliwa Chelsea Mourinho asema yake
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 04, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 04, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment