Jurgen Klopp afunguka kwanini ameamua kujiunga na Liverpool na falsafa atakayoitumia
Kocha mpya wa Liverpool, Jurgen Klopp amefichua kwanini
ameamua kujiunga na wakali hao wa Anfield.
Klopp amesaini mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo pia akija na wasaidizi wake wawili aliokua nao Borussia Dortmund ambao ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Picha nne za mwanzo kocha Jurgen Klopp akitambulishwa Liverpool
Kwenye Interview yake ya kwanza akiwa kama kocha wa Liverpool, Klopp ameiambia tovuti ya klabu kwanini ameungana na timu hiyo na falsafa anayotaka kutumia katika kufundishia.
"Kwanza ningependa kutoa shukrani kwa mmiliki wa klabu ya Liverpool kwa kuonesha kwangu na staff yangu na kutupatia hii nafasi adimu," alisema.
"Wamenipa maono safi na nitashirikiana nao katika kazi na matamanio yao.
"Ninapata msisimko kwa changamoto inayotukabili na nina hamu kuanza kazi na kutekeleza mawazo yetu na namna ya kufanya kazi na hii timu. Hili ni kundi la wachezaji wenye vipaji na bado kuna mengi kumaliza msimu huu.
"Ushindi ni muhimu., lakini ni jinsi gani unashinda na jinsi gani unacheza mchezo. Naamini kucheza katika falsafa ambayo ni ya hisia, imara sana na kasi sana. Timu yangu lazima icheze kwa kukaba
zaidi katika kila mchezo.
"Ni muhimu kua na falsafa ya kuchezea ambayo inaakisi akili yako, inaakisi klabu na inakupa mwongozo mzuri wa kufata. Kimbinu bila shaka, lakini kimbinu kwa moyo mkubwa.
"Liverpool ina wafuasi wa ajabu na Anfield ni nyumba mashuhuri ulimwenguni, ikiwa na anga la ajabu. Nataka kujenga uhusiano mzuri na hawa wafuasi na kuwapa kumbukumbu nzuri. Nadhani wote tunaweza kupeana nguvu na kuianza hii safari pamoja."
Jurgen Klopp afunguka kwanini ameamua kujiunga na Liverpool na falsafa atakayoitumia
Reviewed by Steve
on
Friday, October 09, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment