Propellerads

Ramires afichua hili kuhusu Mourinho na wachezaji wake

                                 


Ramires amesema kua kocha Jose Mourinho bado anapewa
imani kubwa na wachezaji wake kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Mourinho ambaye ameanza vibaya msimu huu kwa matokeo yasiyoridhisha akiwa na point nane pekee katika mechi nane mpaka sasa, alipigiwa kura ya kua na imani naye baada ya matokeo ya kushtukiza dhidi ya Southampton.

Meneja huyo wa Stamford Bridge alisisitiza kua endapo atapoteza imani kwa wachezaji wake ataachana na Blues, lakini hata hivyo Ramires amedai kua Mourinho bado anaaminiwa sana na kikosi.

"Hatujapoteza imani kwa Jose hata kidogo, Kila mtu anamuamini. Tunafikiri ni meneja bora zaidi kwetu." Mbrazil huyo aliiambia The Independent.

"Iko wazi mambo yasipoenda vizuri ambavyo kila mtu anatarajia hua kuna maswali mengi yanaulizwa. Lakini bado tunamuamini.

"Naelewa kikamilifu wapi ametoka na bila kujali alisema nini, kama asingekua anawaamini wachezaji angebwaga manyanga. Lakini hiyo sio kesi. Tuko pamoja.

"Labda ni kosa la wengi kwa sababu mambo yanaenda kinyume na matarajio ya wengi, watu wanaangalia wachezaji na meneja. Lakini tunafanya kazi wote kutoka kwenye hii hali-tunataka kua juu ya msimamo sio mwishoni."



Ramires afichua hili kuhusu Mourinho na wachezaji wake Ramires afichua hili kuhusu Mourinho na wachezaji wake Reviewed by Steve on Friday, October 09, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.