Diego Costa amefafanua kwanini 'haters' wanamchukia Mourinho
'Bad boy' wa Chelsea, Diego Costa amefichua kile anachofikiri
kwanini kocha wake Jose Mourinho anakosolewa sana.
Pamoja na matokeo mabovu, bado Mourinho anaongoza kwa hiki katika Premier League
Fowadi huyo wa zamani wa Atletico Madrid anaamini kua mbinu za Mreno huyo zinapata upinzani sana kutokana na tabia ya uwazi ya Mourinho, amesema husisitiza ukweli ambapo wengine hawapendi kuambiwa,
"Yuko wazi, moja kwa moja,: alisema kwa mujibu wa The Guardian.
"Daima anaongea kile anachofikiri na anachoamini kwamba ni ukweli. Muda mwingine sio kitu ambacho watu wanataka kusikia . Ni jinsi alivyo ndio maana mara nyingine wanamkosoa.
"Wapo mameneja ambao husema kile ambacho watu hupenda kusikia. Nadhani hiyo sio nzuri. Ni bora nikawa na mtu anaenieleza wazi kuliko mtu anaeniambia maneno matamu ambayo ninataka kuyasikia."
Costa pia alisema kua wanasoka wengi watamtaja Mourinho, Pep Guardiola na Diego Simeone kama makocha ambao wangependa kufanya nao kazi.
"Kama ukiuliza mwachezaji milioni meneja gani wanamtaka, watakuja na orodha yenye top three ya Mourinho, Pep Guardiola na Diego Simeone," aliongeza mshambuliaji huyo.
"Ni miongoni mwa sababu nikajiunga Chelsea. Unajua unapokua na meneja mwenye mafanikio , daima ni mbio za ubingwa na daima anacheza klabu bingwa.
"Anashindana kwenye level za juu, anakusaidia kuendelea na kua mchezaji bora. na kukusaidia kupata mataji katika career yako."
Costa amecheza mara nane kwa Chelsea msimu huu huku akifunga magoli mawili pekee.
Diego Costa amefafanua kwanini 'haters' wanamchukia Mourinho
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 10, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment