Wayne Rooney 'Messi ni bora zaidi kuliko Maradona'
Wayne Rooney amefunguka kua Lionel Messi ni bora kuliko
Diego Maradona alivyokua enzi zake.
Mshambuliaji huyo wa Man United amepata kupambana na Messi pale vilabu vyao vilipokutana kwenye fainali ya klabu bingwa mara mbili huku Barcelona wakishinda mara zote.
Rooney anaamini kua Messi ni bora kuliko Maradona japokua hajapata kushinda kombe la dunia, Mkongwe wa Arjentina alichukua kombe hilo mwaka 1986.
Akiwaambia waandishi Rooney alisema "Miaka kadhaa iliyopita, watu walikua wanasema Messi sio kama Maradona kwa sababu hajachukua kombe la dunia. Katika fikra zangu, Messi ni Mchezaji bora kuliko Maradona. Lakini hivyo ndivyo mpira ulivyo"
Messi amepata kuchukua FIFA Ballon d'Or mara nne mpaka sasa katika wakati wake.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Wayne Rooney 'Messi ni bora zaidi kuliko Maradona'
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 05, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment