Propellerads

Kumbe Man United waliamua kumsajili Martial kama mbadala wa Muller



MANCHESTER UNITED waliamua kumsajili Anthony Martial baada ya
dau la pauni mil 60 kwa Muller kukataliwa, hii ni kwa mujibu wa ripoti.

Mashetani hao wekundu walifanya usajili wa kushtukiza kwa Martial akitokea Monaco kwa ada ya £36m ambapo dili lilifanyika siku ya mwisho kufungwa kwa usajili.

Lakini kwa mujibu wa The Sun, Man United walimsajili Martial baada ya ofa ya Muller kukataliwa.

Rais wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alinukuliwa akisema "Ninazungumzia namba ambayo ilikua ni kubwa(pesa), Kama ningekua meneja wa benki ningeamua kuikubali.

"Lakini kama klabu tuliamua kuifungia mlango,na huu mlango utandelea kufungwa. Naweza kuahidi hivyo.


Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24

Kumbe Man United waliamua kumsajili Martial kama mbadala wa Muller Kumbe Man United waliamua kumsajili Martial kama mbadala wa Muller Reviewed by Steve on Saturday, September 05, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.