Propellerads

Samatta afunguka juu ya ufundishaji wa kocha Mkwasa taifa stars




Nyota wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP Mazembe
ya Congo DRC Mbwana Samatta jana baada ya mechi alisema wachezaji wa Stars wanamuelewa sana Kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa na kama mwalimu huyo atapewa muda wa kutosha timu itafanya vizuri.

“Tunamulewa sana kocha, sijui ni kwavile mzawa au vipi, lakini mimi napenda sana mbinu anazozitumia. Nadhani kila mtu ameona mpira tuliocheza leo (jana) japo hatukupata ushindi lakini timu imeonesha matumaini mapya kwa wapenzi wa soka”, alisema Samatta ambaye jana alionesha kiwango kizuri kwenye mechi dhidi ya Nigeria.

“Kutofunga au kupata ushindi kwenye mechi ni sehemu ya mchezo, tulipata nafasi nyingi za kufunga lakini hawatukuweza kupata goli lakini lengo letu lilikuwa ni kupata ushindi tukiwa nyumbani”.

“Nigeria ni timu kubwa, ngumu na tunawaheshimu sana lakini nimependa kiwango tulichokionesha. Naamini kwa baadhi ya makosa ambayo tumefanya, mwalimu na benchi lake la ufundi ameyaona na atayatafutia ufumbuzi ili tunapoingia kwenye mchezo mwingine tuirudie makosa yaleyale”.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Samatta afunguka juu ya ufundishaji wa kocha Mkwasa taifa stars Samatta afunguka juu ya ufundishaji wa kocha Mkwasa taifa stars Reviewed by Steve on Sunday, September 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.