Propellerads

Jose Mourinho noma sana!!, ameingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guinness



Bosi wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameingia kwenye
kitabu cha rekodi cha Guiness cha 2016 akiwa na rekodi tano huku Chris Smalling nae akiingia kwenye kitabu hicho.

Kocha huyo Mreno amevunja rekodi ya  kutofungwa nyumbani kwa muda mrefu zaidi (Miaka 9), most Champions League titles with different teams (akiwa na timu mbili), kocha kijana zaidi kufikisha michezo 100 ya klabu bingwa Ulaya (miaka 49 na siku 12), Point nyingi zaidi katika msimu wa Premier Laegue (point 95), na kutofungwa nyumbani katika michezo mingi zaidi ya Premier League (michezo 77)

"Kiukweli wamenipa tuzo kiasi kwamba nikiweka ofisini inapendeza" Mourinho aliiambia tovuti rasmi ya Chelsea baada ya kupokea tuzo.

"Ni kitu kinachofurahisha sana, kama ukiwa mtoto huwezi kufikiria hata siku moja kama unaweza kua kwenye kitabu cha rekodi cha Guiness.

"Unanijua mimi. Hizi tuzo nimepokea kutokana na kile nilichofanya nyuma inapendeza, lakini kwangu kitu muhimu ni kile nachoweza kufanya kwa baadae"

Mourinho aliungana na beki wa Man United Chris Smalling ambaye ameingia katika kitabu hicho kwa rekodi ya kufunga goli la haraka zaidi la Premier League akiwa kama substitute. Smalling alifunga alifunga dhidi ya Burnley baada ya dakika tno tuu na sekunde tisa alipoingia uwanjani msimu uliopita.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24


Jose Mourinho noma sana!!, ameingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guinness Jose Mourinho noma sana!!, ameingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guinness Reviewed by Steve on Sunday, September 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.